Marekani imemfungulia mashtaka kiongozi wa kundi la Hamas Yahya Sinwar na viongozi wengine wakuu wa kundi hilo la Palestina kwa kupanga na kutekeleza shambulio dhidi ya Israel lililotokea Oktoba tarehe 7 mwaka uliopita.
Miongoni mwa mashtaka yanayowakabili ni kuwauwa raia wa Marekani, kufadhili ugaidi na kutumia silaha za maangamizi dhidi ya watu wasiokuwa na hatia.
Wakati Marekani ikitangaza hatua hiyo, Jeshi la Israeli limeendeleza mashambulio kwenye ukanda wa Gaza hasa kwenye mji wa Rafah , na kusababisha mauaji na kutatiza utoaji wa chanjo ya polio kwa watoto.