Klabu ya Napoli SC imepoteza zaidi ya wafuasi milioni 1.2 kwenye ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa Instagram chini ya saa 24 baada ya mshambuliaji, Victor Osimhen kuondoka katika klabu hiyo.
Mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu ya Italia ‘Seria A’ pia wamefuta picha zote za mshambuliaji huyo raia wa Nigeria kwenye ukurasa huo.
Wakati huo huo klabu ya Galatasaray ya Uturuki ikijukusanyia wafuasi zaidi ya milioni 3 kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii ndani ya saa 24 baada ya nyota huyo kujiunga na klabu hiyo kwa mkopo.