Mwanamuziki Diamond Platnumz usiku wa kuamkia leo kwenye uzinduzi wa Wasafi Festival ametangaza kuwa ndoto yake kubwa ni kuwa tajiri namba moja Duniani na anaamini ipo siku atafanikisha.
Sambamba na hilo ameeleza kuwa Mwaka huu atatambulisha Bidhaa zake mpya ambazo ameahidi zitapendwa sana hivyo anaomba watu wamuunge mkono.
“Naomba vijana wenzangu mlisikilize vizuri. Ndoto yangu kubwa kwenye Maisha ni kuwa tajiri namba moja Duniani. Na ninawathibitishia kuwa nitakuwa tajiri namba moja duniani” alisema Diamond Platinumz
Diamond amekumbushia kuwa hapo zamani alikuwa ana ndoto ya kumiliki Gari aina ya Rolls Royce hatimaye hivi sasa anayo, hivyo anatarajia pia kuwa tajiri namba moja Duniani.