Waratibu wa Mpango wa Okoa Bahari chini ya KONCEPT Group, imeratibu shughuli ya kufanya usafi kandokando mwa bahari ya Hindi katika eneo la ufukwe wa Kawe, Jumamosi, Septemba 7, 2024 kuanzia majira ya asubuhi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, shughuli hiyo ni muendelezo wa jitihada za kulinda mazingira na kuhifadhi fukwe zilizopo nchini kwaajili ya matokeo chanya dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Okoa Bahari Initiative inawakaribisha wadau na wapenda mazingira wote kujumuika pamoja katika shughuli hiyo ya kusafisha mazingira ya fukwe ya Kawe kwa lengo la kusaidia kuweka mazingira salama, safi na yenye afya kwa kila mmoja.