Mwenyekiti wa wafugaji nchini, Mrida Mshoda, amewahimiza wafugaji kote nchini kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura na kuboresha taarifa zao ili waweze kupata haki ya kushiriki katika uchaguzi.
Mrida alitoa kauli hiyo wakati akizungumza wilayani Bunda, mkoani Mara, ambapo alisisitiza kuwa kundi hilo kubwa lina jukumu muhimu la kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo la kuandikisha wapiga kura.
“Sisi wafugaji tunapaswa kuwa mfano katika zoezi hili, kwa hiyo nawahimiza wafugaji kote nchini nendeni mkajiandikishe. Tunapaswa kuiunga mkono Serikali katika zoezi hili,” alisema Mrida Mshoda.
Aidha, Maroche Maroche, mmoja wa wananchi ambaye pia ni mfugaji, alielezea kuridhishwa na namna Tume ya Uchaguzi imeboresha huduma katika zoezi hilo, akibainisha kuwa muda wa kusubiri kwenye vituo umepungua sana, na hivyo kuifanya shughuli hiyo kuwa rahisi na yenye ufanisi zaidi.
“Limekuwa zoezi zuri na lenye muda mfupi; ukifika ni muda mchache unaondoka, kwa hiyo kipindi hiki tume imejitahidi sana,” alisema Maroche.
#KonceptTvUpdates