Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu, amewataka wabunge kutokuwa na hofu ya kurudi majimboni na kuwahimiza kuzungumzia mafanikio yaliyopatikana kupitia miradi mbalimbali.
“Niwapongeze kwa kazi nzuri mliyofanya, mmeonyesha uwezo na sifa za kurudi tena bungeni mwaka 2025,” alisema Zungu.
Zungu aliwataka wabunge kutokata tamaa kwa changamoto zozote wanazoweza kukutana nazo na kuwaelekeza waende majimboni na kujivunia mafanikio ya serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
“Msirudi majimboni na hofu, nendeni mkizungumzia maendeleo, msirudi na unyonge,” aliwasisitiza.
Zungu alitoa kauli hiyo Septemba 6, 2024, jijini Dodoma wakati wa kuahirisha mkutano wa 16 wa Bunge hadi Oktoba 29, 2024.
#KonceptTvUpdates