Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, amefichua sababu zilizomfanya serikali kumfukuza nchini mchungaji maarufu anayejulikana kama ‘Kiboko ya Wachawi.’ Kwa mujibu wa Masauni, mchungaji huyo aliondolewa nchini baada ya kukiuka sheria za usajili na kushiriki katika vitendo vilivyo kinyume na mafundisho ya dini.
Waziri Masauni amesema kuwa ameshuhudia mchungaji huyo, ambaye kwa sasa yupo nje ya nchi, akisambaza video za kuthibitisha kwamba alikuwa akijihusisha na vitendo vya ulaghai. Mchungaji huyo amekuwa akiwaaminisha waumini kwamba miujiza inaweza kuwafanya kuwa matajiri, na kuwatoza watu fedha kwa njia zisizokubalika, jambo ambalo ni kinyume na mafundisho ya dini.
Masauni alisisitiza kuwa serikali haiko tayari kuvumilia vitendo vyovyote vya udanganyifu au utapeli vinavyovunja sheria na kwenda kinyume na misingi ya imani za kidini. Mchungaji huyo aliondolewa nchini ili kulinda ustawi wa raia na kuhakikisha ufuataji wa sheria na taratibu za usajili wa viongozi wa kidini.
#KonceptTvUpdates