Leo mapema, Waratibu wa Mpango wa OKOA BAHARI, Koncept Group kwa kushirikiana na OCEAN LIFE GUARD pamoja na wadau wengine wa Mazingira wamefanikisha zoezi la kufanya Usafi kwenye eneo la Fukwe za Kawe (Kawe Beach) ikiwa na lengo la kuweka fukwe katika hali ya usafi na kuhifadhi mazingira Kiujumla.
Zoezi hilo limeongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Koncept Group Krantz Mwantepele kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mzimuni (pembezoni mwa fukwe za Kawe) Raiya Nassrr Amour, Kiongozi Serikali ya Mtaa Fredrick Kavaga, Afisa wa Afya na Mazingira Joachim Kilawe pamoja Wadau wengine wanaofanya shughuli za uvuvi na biashara ndogondogo katika Viunga vya Fukwe ya Kawe.
“Tunatekeleza mpango huu endelevu wa kuweka na kutunza Mazingira kwa kufanya usafi katika fukwe za Bahari tukinza na fukwe ya kawe (Kawe Beach) ili kuunga mkono jitihada za Serikali za Kuhifadhi Mazingira ya hapa nchini Tanzania na Dunia kiujumla, licha ya kwamba leo tumewasili na kushiriki watu wachache na tumefanya kadri ya uwezo wetu, tunatarajia msimu ujao kushirikisha wadau wengi zaidi kwenye hili suala ili kuleta tija zaidi kwenye suala zima la uhifadhi wa Mazingira” ameeleza Krantz Mwantepele
Pia Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Raiya Amour ameipongeza Kampuni ya Koncept Group kwa kuanzisha na kutekeleza mpango wa “OKOA BAHARI” kwa vitendo kwa kuwa inachangia kwa ukubwa kwenye suala zima la Uhifadhi wa Mazingira yetu hasahasa maeneo ya fukwe za bahari ambayo hupokea taka nyingi kutoka sehemu mbalimabali.
#KonceptTvUpdates