Shirika la Agakhan limetoa bidhaa za Afya na vifaa vya kujikinga na maambukizi (Personal Protectove Equipment) dhidi ya ugonjwa wa homa ya Nyani (M – POX) vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 200.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mohamed Mchengerwa tarehe 07.09.2024 kwenye kituo cha Afya Ikwiriri Kilichopo wilayani Rufiji mkoani Pwani.
Akizungumza wakati wa tukio hilo Afisa Uhusiano wa Agakhan Juma Dosa amesema wameamua kuunga mkoni jitihada za Waziri Mchengerwa za kuboresha Afya za Wanarufiji na kwa kufanya hivyo wamekuja na bidhaa za Afya na vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ta shilingi Mil. 200 kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya M-Pox.
Dosa aliongeza kuwa misaada hiyo ileenda sambamba na huduma za uchunguzi wa magonjwa ya Kansa ya ziwa, mlango wa kizazi pamoja na Tezi Dume hapa Ikwiriri na huduma hizo zitatolewa bura kwa muda wa siku 2.
Akizungumza baada ya kupokea bidhaa za Afya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amewashukuru Aghakan kwa mchango wao katika huduma za Afya Rufiji na ametaka wananchi wa Rufiji kutumia fursa hiyo kufika kwenye Kliniki kwa ajili ya uchunguzi wa Afya zao.
Aidha amemuagiza Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Dkt. Rashid Mfaume kufanya mgawanyo sahihi wa vifaa vya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa M-Pox na kuvipeleka kwenye maeneo ya mipakani.