Waziri wa Maji Jumaa Aweso (Mb ametembelea Mradi wa Maji wa Mabadiliko ya Tabia Nchi Simiyu unaotumia chanzo cha ziwa Victoria kwa thamani ya kiasi cha zaidi ya Bilioni 400 wilayani Bariadi mkoa wa Simiyu
Mradi utakaonufaisha wilaya za Bariadi, Busega, Itilima, Meatu na Maswa.
Waziri Aweso amekagua hatua ya mradi na kutoa maelekezo mahsusi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mkandarasi wa mradi anafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kazi kwa muda uliopangwa kwasababu fedha yote ya mradi ipo.
Aweso katika ziara hiyo ameambatana na Naibu Waziri wa Maji Mhe Mhandisi Kundo Mathew (Mb) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Kenan Kihongosi, na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri.
Ameelekeza wananchi na vijana wote wenye sifa ya kufanya kazi kutoka kwenye maeneo ya ujenzi wa mradi utaratibu ufanyike waweze kupata kazi.
Katika hatua nyingine Waziri Aweso amemteua Mhandisi Emmanuel Luesetula ambae anakaimu ya nafasi ya Meneja wa Mkoa – RUWASA kuwa Mhandisi wa Maji Vijijini mkoa wa Simiyu.