Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Dk.Hussein Ali Mwinyi amerejea Zanzibar, baada ya kumaliza ziara yake nchini Indonesia na kushiriki katika Sherehe za Miaka 50 ya siku ya Ushindi nchini Msumbiji.
Dk.Mwinyi amepokelewa na Makamu wa Pili wa Rais Mhe Hemed Suleiman Abdulla pamoja na Viongozi wengine wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
Vilevile Dk. Mwinyi amepata fursa ya kuongea na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari na kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika ziara hiyo.
#KonceptTvUpdates