Safari ya Treni ya Mwendokasi inayosafiri kati ya Dar es Salaam na Dodoma ilisita kwa saa kadhaa usiku wa kuamkia leo, Septemba 10, 2024, katika eneo la Ngerengere. Tukio hilo liliwashtua abiria, ambapo baadhi yao walijirekodi video wakionesha kutokuwa na uhakika wa muda watakaotumia kusubiri.
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeomba radhi kwa kuchelewa huko, likieleza kuwa kusimama kwa treni kulitokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao. Miongoni mwa changamoto zilizochangia ni kupishana na treni nyingine iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro, hali iliyopelekea kuchelewa kwa safari.
Akizungumza na AyoTV, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa TRC, Jamila Mbarouk, alisema: “Changamoto hizo baadaye zilitatuliwa na huduma za usafirishaji ziliendelea kama kawaida. TRC inaomba radhi kwa usumbufu uliowapata abiria na tunaahidi kuzifanyia kazi changamoto hizo ili kuboresha huduma zaidi.”
Shirika hilo limeendelea kusisitiza kuwa linafanya jitihada za kuhakikisha usafiri wa reli unakuwa wa haraka na bora kwa abiria wake, huku likijitahidi kutatua changamoto zinazoibuka kwa wakati.
Cc; AyoTv
#KonceptTvUpdates