Zaidi ya wahalifu 1,700 nchini Uingereza na Wales watatolewa gerezani mapema leo kama sehemu ya mpango wa serikali wa kupunguza msongamano magerezani. Hatua hii inatekelezwa baada ya serikali ya Labour kuingia madarakani baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Julai, ingawa maafisa walikuwa tayari wamepanga hatua hiyo kabla ya chama cha Conservative kumaliza muda wake madarakani.
Katika orodha ya wahalifu wanaopaswa kuachiliwa leo, 1,000 kati yao ni wale ambao wanastahili kuachiliwa kawaida ndani ya wiki moja. Mpango huu unaruhusu wafungwa kuachiliwa baada ya kukamilisha 40% ya kifungo chao, tofauti na asilimia 50 iliyokuwa inatumika awali, kwa lengo la kuhakikisha vitanda 5,500 vinakuwa wazi katika magereza.
Hata hivyo, sera hii haitatumika kwa wahalifu waliopatikana na hatia ya makosa ya ngono, ugaidi, unyanyasaji wa nyumbani, au baadhi ya makosa ya vurugu. Hatua hii ni sehemu ya jitihada za serikali ya Labour kupunguza msongamano magerezani na kuboresha hali ya magereza nchini Uingereza na Wales.
#KonceptTvUpdates