Wizara ya Mambo ya Nje ya Ukraine imemuita Balozi mdogo wa Iran Shahriar Amouzegar kwa mazungumzo kuhusu taarifa zinazodai kuwa Tehran inapewa makombora ya masafa marefu kwa ajili ya Urusi. Taarifa hiyo imeelezwa kupitia mtandao wa Telegram kwamba Ukraine imetoa onyo kali kwa Balozi Amouzegar kutokana na taarifa aliyoitoa kuhusu uwezekano wa kutoa makombora hayo, huku ikisisitiza kuwa uwepo wa ukweli huo unaweza kuathiri vibaya uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
Katika taarifa nyingine, Ikulu ya Marekani (White House) imeeleza kushtushwa na taarifa za vyombo vya habari vya Magharibi zinazosema kuwa Iran inatuma makombora kwa Urusi kwa matumizi dhidi ya Ukraine. Taarifa hii ilitolewa mwishoni mwa juma lililopita kupitia shirika la habari la Sauti ya Amerika (VOA), ikisisitiza kuwa taarifa hizo hazijathibitishwa rasmi.
Gazeti la Wall Street Journal liliripoti Ijumaa iliyopita kuwa maafisa wa Marekani na Ulaya, ambao majina yao hayakufichuliwa, wamegundua kuwa Iran inatuma makombora ya masafa marefu kwa Urusi. Hata hivyo, Kremlin na maafisa wa Iran wamekanusha vikali taarifa hizi, huku maafisa wa Iran wakithibitisha Jumatatu, Septemba 9, 2024, kwamba hakuna makombora yaliyotolewa kwa Urusi.
#KonceptTvUpdates