Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Septemba 11, 2024 amezindua Taarifa za Maboresho ya Mazingira ya Uwekezaji na Biashara pamoja na Nyenzo za Usimamizi wa Uwekezaji, katika Ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es salaam.
Taarifa na nyenzo hizo zitasaidia katika kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa kutoa mwongozo, kuboresha taratibu na kuongeza ufanisi.
Aidha, Nyenzo hizo zitasaidia katika kupima maendeleo, kutatua changamoto na kuhakikisha kwamba uwekezaji unakua katika mazingira rafiki na yenye ushindani.
Viongozi wengine wanaoshiriki katika tukio hilo ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Stanslaus Nyongo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Taarifa za Maboresho ya Mazingira ya Uwekezaji na Biashara pamoja na Nyenzo za Usimamizi wa Uwekezaji, katika Ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es salaam, Septemba 11, 2024. kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo na kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Stanslaus Nyongo
Aidha, katika uzinduzi huo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko pia alishiriki.