Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mary Maganga, amelitaka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kuendelea kuboresha ubora wa huduma wanazozitoa kwa wananchi ili kuendana na viwango vya kimataifa vya utoaji huduma bora (ISO certification).
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Cheti cha Ithibati ya huduma bora kwa viwango vya kimataifa kwa WCF, jijini Dar es Salaam, Maganga alibainisha kuwa maboresho ya mfuko huo yanapaswa kuzingatia mahitaji na matarajio ya wateja. Alisema, wafanyakazi wanapaswa kupata fidia stahiki wanapopata madhara kutokana na ajira zao.
Alisisitiza kuwa, “Ni muhimu kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma ili kuhakikisha waajiri wanapata urahisi wa kujisajili kwa hiari badala ya kushurutishwa na sheria.”
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dk. John Mduma, alieleza kuwa mafanikio hayo yametokana na uwekezaji mkubwa katika teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama), huku akiwahimiza wadau wa mfuko huo kutumia huduma za mtandao.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Viola Masako, aliipongeza WCF kwa jitihada zake za kuleta mabadiliko chanya katika utoaji wa huduma kwa kuzingatia viwango vya kimataifa, akisema kuwa ni ishara ya uwajibikaji wa hali ya juu.
#KonceptTvUpdates