Wamiliki wa vyombo vya moto nchini wametakiwa kuhakikisha madereva wa vyombo hivyo wanafuata sheria za usalama barabarani na kuacha mara moja tabia ya kuendesha magari ya abiria na mizigo bila kukagua magari wanayoyaendesha ili kubaini mapungufu yaliyopo katika vyombo hivyo.
Kauli hiyo imetolewa Septemba 17, 2024 na Mkuu wa Operesheni Kikosi cha Usalama barabarani nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Nassor Sisiwaya alipokuwa Kituo cha Ukaguzi wa Magari