Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewatembelea wagonjwa na kuwafariji katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mjini Lumumba.
Wagonjwa waliotembelewa ni Ndugu Mbaraka Omar Kassongo, Afisa Tawala wa Wilaya ya Kusini Unguja; Mzee Haruna Juma Hassan, mstaafu wa Utumishi wa Umma; na Mzee Ibrahim Ali Suleiman.
Rais Dk. Mwinyi amewatakia heri na kuwaombea kupona haraka.
Rais Dk. Mwinyi amekuwa na utaratibu wa kuwafariji wagonjwa.