Kupitia mitandao yake ya Kijamii, aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mch. Peter Msigwa ameonesha kushangazwa na mwitikio mdogo wa watu waliokuwa wakihamasisha wananchi kujitokeza kwenye maandamano ya Chadema yaliyokuwa yamepangwa kufanyika Septemba 23, Jijini Dar es salaam.
“Watu wanapenda kujiita makamanda hapa kwa mitandao (keyboar heros) wamemuacha mwamba anaandamana pekee yake hata watu hamsini hawakufika magomeni.Wapi mwita , Catherine, maranja, Lutembeka, mwenyekiti wa kanda ya Nyasa wapi Taita! Wapi Big Mungai!?…. Hata kama mtachukia hii inasema kitu.
Tuna Tanzania ya kuijenga. Niltegemea wale watoa matusi hapa wangekuwa wa kwanza kufika magomeni”
Wakati Msigwa akisema hayo mtumiaji mwingine wa mitandao ya Kijamii Onesmo Mushi, ameandika;
“Mimi nina theory kwamba pengine Mhe. Mbowe hakutaka wafuasi wa CHADEMA watunishiane misuli na polisi (kwa kuogopa kuwa silaha za jeshi la polisi na kutokujali kwao kungeweza kumwaga damu za wengi wasiokuwa na hatia) na hivyo akaamua asimobilize watu au akapitisha taarifa chini chini watu wasijitokeze akiamini kuwa yeye mwenyewe angetosha kufanikisha lengo pasipo kuathiri wafuasi wengi?
Hii ni moja ya strategy zilizotumiwa na wanajeshi wengi zamani; rejea kisa cha Achilles na Hector pale kwenye geti la Troy au hata Daudi na Goliathi kwenye biblia. Ni nadharia tu, sitaki kukubaliana kirahisi kuwa “watu hawakutoka kwa sababu Mbowe ushawishi” wakati juzi tu mwezi wa kwanza walitoka kwa maelfu, achilia mbali vitisho vilivyokuwepo.” Amesema.