Mwanamitindo maarufu duniani Naomi Campbell (54), amepigwa marufuku ya miaka 5 kuwa Mdhamini wa Shirika la hisani alilolianzisha kwa ajili ya kutoa misaada ya kupunguza umasikini.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya uchunguzi wa kina kupata ushahidi wa kutosha wa matumizi mabaya ya fedha ndani ya Shirika hilo lijulikanalo kama “Fashion for Relief”.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya kugundulika kuwa amekuwa akiwapa walengwa pesa ndogo sana kati ya Mamilioni ya Dola za Kimarekani alizokuwa akizikusanya kuwasaidia wahitaji.
Pesa hizo zimekuwa zikikusanywa kupitia shughuli mbalimbali zilizojaa watu mashuhuri. Uchunguzi uliofanywa na Baraza la Mashirika ya hisani Uingereza umebaini kuwa baadhi ya pesa hizo zimekuwa zikitumika kwa gharama za kifahari kama mahotelini, ulinzi na mishahara. Pamoja na mwanamitindo huyo, wadhamani wenzake wawili nao wamepigwa marufuku hayo.