Hatua ya hivi karibuni ya kukamatwa kwa mwanamuziki na mfanyabiashara wa nchini Marekani, Sean Combs maarufu Diddy, imegeuka fursa kwa mwanamuziki 50 Cent pamoja na Netflix ambao wanetangaza kutoa tamthilia kuhusu biashara ya usafirishaji wa binadamu, ulaghai na tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi ya gwiji huyo wa muziki wa Bad Boy Records.
Katika taarifa yake 50 Cent pamoja na Alexandria Stapleton wametaja mtiririko wa matukio utakavyokuwa ndani ya tamthilia hiyo.
“Hii ni hadithi yenye athari kubwa ya kibinadamu, ni simulizi changamano iliyochukua miongo kadhaa…Tuna lengo thabiti katika kujitolea kwetu kutoa sauti kwa wasio na sauti na kuwasilisha mitazamo ya kweli na isyofahamika, madai hayo yanasumbua wana jamii, tunawahimiza wote kukumbuka kuwa hadithi ya Sean Combs sio hadithi kamili ya hip-hop na utamaduni wake”. amesema Alexandria Stpleton
50 Cent atakuwa mtayarishaji mkuu wa kutengeneza mfululizo wa matukio hayo kupitia G-Unit Filamu na Televisheni na Alexandria Stapleton atakuwa Muongozaji Mkuu.