Costco imekanusha madai kuwa Sean “Diddy Combs hununua mafuta ya watoto kwa wingi kutoka kwenye maduka yao, kufuatia tuhuma zilizohusishwa na mashtaka yake yanayomkabili.
Mwanasheria wa rapa huyo Mac Agnifilo alisema kuwa kiasi kikubwa cha mafuta ya watoto kilichopatikana nyumbani kwa Diddy kilikuwa ni matokeo ya mazoea ya kununua kwa wingi, akitaja eneo la karibu.
Costco hata hivyo imekanusha haraka jambo hili, ikisema kwamba hawakumuuzia Diddy mafuta yoyote ya watoto, kwani si miongoni mwa bidhaa wanazohifadhi katika maeneo yao yoyote huko Marekani.