Jozi za viatu ‘Black Air Force 1’ zilizotumiwa na Kendrick Lamar kwenye Music Cover ya wimbo wake ‘Watch the Party Die” za wekwa sokoni kwa kiasi cha pesa $75,000 sawa Tsh 205 Milion.
Wauzaji wa eBay ambao waliweka sokoni viatu hivyo pia wameorodhesha t-shirt zenye picha ya viatu hivyo zinazouzwa $35 sawa na Tsh 95,790.
Watch the Party Die ni wimbo wa Lamar aliouachia Instagram siku 3 baada ya kutangazwa kuwa atatumbuiza kama msanii nyota kwenye jukwaa la ‘SuperBowl Half Time Show 2025’