Siku ya kwanza ya maonyesho ya S!TE 2024 yalianza kwa ari ya juu kwa Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi kuongoza sherehe za ufunguzi akiambatana na wadau wa sekta ya utalii duniani.
Mijadala mbalimbali muhimu ilijadiliwa na mawazo ya kibunifu tayari yanapeleka mbele mustakabali wa sekta ya usafiri. Nawe unaweza kuwa sehemu ya mabadiliko haya kwa kuhudhuria maonyesho haya kwa kutembelea viwanja vya Mlimani City ambapo siku ya pili ikiwa inaendelea na kesho kesho pia kushuhudia kile ambacho S!TE imekuandalia msimu huu.