Shirika la Global Water Center kutoka Jimbo la South Carolina nchini Marekani limeweka bayana mpango wake wa kushirikiana na RUWASA katika kutoa mafunzo kwa Wataalamu katika Usimamizi wa Skimu za Maji zinazotumia Nishati ya Jua na Usimamizi wa Maji chini ya Ardhi. Hayo yamewasilishwa na Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo Thomas Johnston wakati RUWASA ilipoalikwa katika mkutano ulioandaliwa na Shirika hilo na kufanyika Mjini Unguja, Zanzibar tarehe 22 Novemba, 2024.
Naye Mhandisi Clement KIVEGALO ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA ametanabaisha kuwa mafunzo hayo kwa Wataalamu katika Sekta ya Maji ni muhimu sana katika kuwezesha uendelevu wa miradi inayojengwa na Serikali ya Tanzania.