Rapa wa kundi la Young Money Michael Ray Nguyen-Stevenson, maarufu zaidi kama Tyga ameonyesha ni jinsi gani hasikii wala haoni zaidi ya Kylie Jenner.
Kylie Jenner ambaye ni mtangazaji wa televisheni na Mwanamitindo alisheherekea siku yake ya kuzaliwa Agosti 9 akiwa anatimiza miaka 18 kwani amezaliwa Agosti 10 1997. Akiwa anasheherekea na familia yake, Jenner aliduwaa baada ya kutoka nje ya ukumbi na kukutana na Ferrari mpya kabisa ikiwa imepambwa ua jekundu juu yake kama zawadi ya siku ya kuzaliwa kutoka kwa Tyga.
Tyga ameamua kukata mzizi wa fitina kwa kuipa dunia ukweli kwamba mapenzi yao ni ya kweli kwani gharama aliyoitumia ya $320,000 kumnunulia Jenner Ferrari si haba.