Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP DANIEL SHILA ameitaka jamii kuacha tabia ya kutumia vibaya mitandao ya kijamii na kurusha picha zenye kuleta taharuki kwa wananchi.
Akitoa ufafanuzi huo ofisini kwake Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja alisema video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikionesha watu jamii ya Kimasai wakiwashambulia walinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi ni kwamba tukio hilo lilitokea muda mrefu uko nyuma na tayari lilishachukuliwa hatua za kisheria.
Wakati huo huo Kamanda Shila amewatunuku vyeti na zawadi Askari 10 waliofanya vizuri Zaidi mwaka 2023 nakupelekea Mkoa huo kuendelea kuwa na amani na utulivu na kufanikisha watuhumiwa wa uhalifu kukamatwa na kufikishwa mahakamani.
#KonceptTvUpdates