Klabu ya Young Africans imepanga kuleta utofauti sio kama ilivyozoeleka kwa kutumia fursa ya uwekezaji kwenye soka la mpira wa miguu kuwa wa chachu ya mabadiliko chanya kwa mashabiki na wadau mbalimbali
Kupitia mkutano na waandishi wa habari Afisa Habari wa Yanga amefunguka kudhihirisha nia ya klabu hio kwenye dhima nzima ya kuleta mabadiliko hayo kupitia soka.
𝐏𝐑𝐄𝐒𝐒 “Nimeona dalili kuwa tumeanza kuzoeleka vibaya, hivi karibuni kuna namna msimamo wa ligi ukiwekwa tunakwazika. Sio kawaida yetu sisi kuwa kwenye nafasi hizo. Wananchi, leo tufike kwa wingi Uwanja Azam Complex, Chamazi kuhakikisha tunarejea kwenye nafasi yetu” Ally Kamwe
“Leo rasmi tumeingia kwenye wiki ya anniversary ya miaka 89 ya Klabu hii kubwa Tanzania, kuelekea kilele cha Birthday ya Young Africans SC tarehe 11 mwezi huu wa pili, safari hii tuna mambo makubwa. Hii ni wiki yetu wenyewe” Ally Kamwe
“Kesho Young Africans SC tutakwenda kusaini mkataba na Hospitali kubwa sana duniani, ikiwa na lengo la kumnufaisha shabiki wetu kwenye masuala yanayohusu afya yao. Klabu kubwa lazima iwaze kwa ukubwa namna gani Mwanachama wake atanufaika na Klabu kubwa.
“Siku ya Jumatano, pale makao makuu ya Klabu Jangwani, tunakwenda kuzindua upya ofisi zetu. Uongozi wa Klabu yetu umefanya ukarabati wa kihistoria. Ukarabati huo umeifanya Klabu ya Young Africans SC kuwa na ofisi bora zaidi AFRIKA MASHARIKI NA KATI.” Ally Kamwe