![Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na kusoma](https://scontent.fdar7-1.fna.fbcdn.net/v/t39.30808-6/426378920_771415311689903_7675481504584493804_n.jpg?_nc_cat=101&ccb=1-7&_nc_sid=dd5e9f&_nc_eui2=AeE9KrNvdzKsRm0X3RtQjbJciuLBMh-3PjOK4sEyH7c-M63S6CU0NSeJCbIlNmYiIApvX-quowXflpNxIcHC-NKU&_nc_ohc=XSP_Zl-vbh4AX-2rrs4&_nc_ht=scontent.fdar7-1.fna&oh=00_AfAh8Gf5_EKvYgY_59gu3f-D7Dy_3A7-DH8LZP7ThBMd-w&oe=65D25E34)
Akizungumza baada ya kujionea mfumo huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Denis Londo amesema wameridhishwa na mfumo huo huku akiipongeza Serikali kwa kuja na teknolojia hiyo ambayo inakwenda kukuza kiwango cha elimu nchini.
“ Niipongeze Serikali yetu inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta ya elimu, tumejionea shule nyingi zikijengwa, uwekezaji wa elimu bila malipo hadi kidato cha sita na sasa teknolojia hii ya wanafunzi wa shule nyingine kushiriki kipindi cha masomo na wenzao waliopo Kibaha Sekondari.”
“Rai yetu kama Kamati ni kuitaka Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuusimamia kikamilifu mfumo huu ili uweze kuleta tija kwa wanafunzi wetu nchini. Lakini niwatake wanafunzi hawa wanaonufaika na mfumo huu kuutumia kikamilifu ili waweze kufaidika nao kwenye masomo yao na kupata matokeo mazuri,” amesema Mhe. Londo.
![Inaweza kuwa picha ya Watu 2 na watu wanaosoma](https://scontent.fdar7-1.fna.fbcdn.net/v/t39.30808-6/426351073_771440298354071_8850369857230590958_n.jpg?_nc_cat=101&ccb=1-7&_nc_sid=dd5e9f&_nc_eui2=AeHLPTNEPD-LCpa9QmiGYHfd2QYC2ckhzZDZBgLZySHNkG-a8L4fQDPQBfsyW7xW9mN2UHVdoHf4bO-voGQdiqp6&_nc_ohc=pOBf0zBqzuQAX_3PxKk&_nc_oc=AQmGZrzae5OlockbfaIsX-rcU95C1tWds2deROKhtNpjtJbtrAp83ycIvxVSmNDdULk&_nc_ht=scontent.fdar7-1.fna&oh=00_AfBVcZcbsgQoMEwkzKdwGnFNs7GOgNh_o8BIix4Rqlw4ow&oe=65D26EC8)
#KonceptTvUpdates
![Inaweza kuwa picha ya Watu 4 na watu wanaosoma](https://scontent.fdar7-1.fna.fbcdn.net/v/t39.30808-6/426362883_771415431689891_314509091598868045_n.jpg?_nc_cat=101&ccb=1-7&_nc_sid=dd5e9f&_nc_eui2=AeEn-nuhlMVpclETmWkW6sd4XJi2WGkqNKRcmLZYaSo0pJzgwXnGcqbSVFjtTswos4ceThm9OSyNUiuyIQ5D2n6T&_nc_ohc=_gedzMYToYIAX84Y26D&_nc_ht=scontent.fdar7-1.fna&oh=00_AfD--kfljrvlHRY3jne8xjcnzcEZqri7oAObS4B7vOoRDg&oe=65D20644)