Mahakama ya Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu mbele ya Hakimu Mfawidhi Mhe.C.G Rugumila imemuhukumu kijana Steven Leonard,miaka 19,kinyozi na mkazi wa kijiji cha Bushigwamala kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kumshawishi na kubaka mwanafunzi wa kike wa kidato cha tatu wa Shule ya Sekondari Kalemela.
Hukumu hiyo imesomwa Machi,5 2024 baada ya mahakama kujiridhisha kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo tarehe 28.07.2023 katika kijiji cha Masanza ambapo alimtorosha binti huyo chini ya uangalizi wa wazazi na kwenda kuishi nae kama mke wake kinyume cha sheria.
Kijana huyu alifika kijiji cha Bushigwamala akiwa anafanya kazi za kunyoa katika saluni na kuingiza nyimbo kwenye simu .
#KonceptTvUpdates