Vodacom Tanzania yashiriki Mkutano wa 21 wa Taasisi za Kifedha Ulioandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania Kujadili Uimarishaji wa Sekta za Kifedha Kukabiliana na Changamoto za Kiuchumi Jijini Arusha.Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa mkutano wa 21 wa Taasisi za Fedha ulioandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania kujadili uimarishwaji wa sekta za kifedha ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi mwishoni mwa wiki jijini Arusha. Vodacom Tanzania inajivunia kuleta huduma jumuishi za kifedha nchini kwa miaka 15 sasa ikitumiwa na Watanzania zaidi ya milioni 20.
Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni (katikati) akizungumza wakati wa mkutano wa 21 wa Taasisi za Fedha ulioandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania kujadili uimarishwaji wa sekta za kifedha ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi mwishoni mwa wiki jijini Arusha. Vodacom Tanzania inajivunia kuleta huduma jumuishi za kifedha nchini kwa miaka 15 sasa ikitumiwa na Watanzania zaidi ya milioni 20.
Washiriki wakiendelea na mijadala wakati wa mkutano wa 21 wa Taasisi za Fedha ulioandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania kujadili uimarishwaji wa sekta za kifedha ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi mwishoni mwa wiki jijini Arusha.