Ikiwa ni Siku ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani, inatukumbusha kuwa tabasamu lenye afya ni uwekezaji tosha wa maisha yote! Hapa kuna njia 5 za kutunza afya yako ya kinywa na meno. Afya yako ya kinywa huathiri ustawi wako kwa ujumla, kwa hivyo wacha tufanye usafi wa kinywa na meno kuwa tabia ya kila siku.
1. Piga mswaki meno yako mara mbili kwa siku.
Matumizi ya Kinywa katika Ulaji huacha mabaki ya chakula kyenye meno na baadhi ya sehemu ambayo yakiendelea kuwepo kwa muda mrefu huleta harufu mbaya na kuunda kemikali zinazopelekea pia meno kuoza. Hivyo ukipiga mswaki walau mara mbili husadia kuondokana na kadhia hiyo.
2.Muone daktari wako wa Meno mara kwa mara kwa uchunguzi na usafishaji
3. Kula chakula chenye uwiano mzuri
4. Epuka kula vyakula vyenye sukari nyingi
5. Sukutua mdomo wako kila mara ili kujiweka katika hali ya usafi zaidi.
NOTE: Jitaidi kuongea na Kutabasamu mara nyingine kuruhusu mzunguko wa hewa safi kuingia na kutoka kupitia kinywa chako.
Je wewe huwa unafanyaje kuhakikisha unatunza afya ya kinywa chako?
Toa maoni yako kuhusiana na hili!