Muigizaji mkongwe wa Nollywood nchini Nigeria, Amaechi Muonagor amefariki Dunia akiwa anapatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu na kufeli kwa figo yake kukielezwa kuwa chanzo cha kifo chake.
Siku chache hapo nyuma habari nyingi zilisambaa mtandaoni kwa mfumo wa video zikimuonyesha muigizaji huo akiomba watu wamchangie fedha ili asafiri nje kwaajili ya matibabu lakini kabla hatua ya uchangiaji haijakamilika ameripotiwa kuwa amepoteza maisha.
Muigizaji huyo amefariki akiwa na miaka 62 hivyo, kulingana na alama aliyoiacha kwenye Tasnia ya Filamu kupitia uigizaji wake wenye ucheshi, umeacha simanzi kubwa kwa mashabiki zake
#KonceptTvUpdates