Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Awadhi Juma Haji na Kamishna wa Polisi Jamii CP Faustine Shilogile kwa pamoja wameendelea na Ziara ya kikazi katika Mkoa wa Polisi Tarime Rorya na kuzungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mrwambe Kata ya Kemambo Wilaya ya Kipolisi Nyamwaga, Kijiji ambacho kimepakana na Mgodi wa Barrick North Mara uliopo Nyamongo.
Kabla ya kuzungumza na Wananchi hao aliwapa nafasi ya kuuliza maswali na kutoa maoni na ushauri nini kifanyike hili kudhibiti matendo ya uvunjifu wa sheria.
Kamishna wa Polisi Awadhi Juma Haji amewaeleza kuwa, Jeshi la Polisi alitokuwa na muhali na yeyote anayevunja sheria kwa kufanya uvamizi katika mgodi wa Barrick North Mara na yeyote atakayebainika kufanya uhalifu atakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
#KonceptTvUpdates