Zoezi la urejeshaji wa miundombinu ya barabara kuu ya Lindi – Dar es Salaam katika eneo la Somanga Mkoani Lindi ukiendelea ambapo timu ya wataalam kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS) wanasimamia zoezi hilo kikamilifu ili kuruhusu mawasiliano kurejea kwa haraka.
Aprili 5,2024 Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa aliongea na wananchi waliokwama katika eneo hilo na kutoa taarifa yakuwa urejeshaji wa miundombinu ya barabara hiyo unatarajiwa kukamilika ndani ya saa 72 na kuweza kuruhusu magari na wananchi kupita katika eneo hilo.