Msaanii wa vichekesho nchini Tanzania maarufu sana kwa jina la Kitale, ameibua ubunifu wa kurekodi vichekesho vya sauti ambavyo vimetokea kukubalika sana.
Vichekesho hivyo vinavyokwenda kwa jina la Mkude Simba vimefanya hata kitale mwenyewe kuitwa Mkude Simba anapokatiza mitaani.
Akizungumza na mtandao wa Bongo5 Kitale amesema amepata mafanikio makubwa baada ya mitandao ya simu kusaini naye mikataba ili kutumia audio za Mkude Simba kama miito ya simu.
Ameongeza kuwa makampuni mbalimbali yamevutiwa na kazi zake na wanamuhitaji kufanya kazi na yeye kwa kutambua kukubalika kwa audio za Mkude Simba, amepanga kurekodi video na hatimaye kuja na filamu ya Mkude Simba.
Harkati 360 inamtakia kila la kheri bwana Kitale.