Mke wa Bobby Brown anatarajiwa kumpatia mwanamuziki huyo mtoto wao wa pili, wakati binti yake mkubwa Bobbi Kristina akiendelea kupigani uhai wake hospitali.
Mke wa nyota huyo wa R&B Alicia Etheredge anaujauzito wa miezi minne, kwa mujibu wa taarifa za jarida la TMZ, ilizozipata kwa ndugu wa karibu.
Hata hivyo habari hizo nzuri zinakuja wakati binti yake wa maika 21 aliyezaa na Whitney Houston, Bobbi Kristina akiwa kalazwa hospitali ya Chuo Kikuu cha Emory, akiwa hajitambui baada ya kukutwa bafuni akiwa kapoteza fahamu.
Bobbi Kristina akiwa na baba yake Bobby Brown