Mwanamuziki Ali Kiba akizikonga nyoyo za mashabiki waliofurika Dar Live katika shoo yake ya Mwana Dar Live iliyokuwa ikipigwa kwa ‘Live Band’.
Ali Kiba na mdogo wake Abdul Kiba wakichekecha na kucheketua.
Mashabiki wa Ali Kiba wakishow love.
Ali Kiba na mdogo wake Abdul Kiba wakizidi kuwapagawisha mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live Sikukuu ya Pasaka.
Mashabiki wa Ali Kiba wakicheza staili mpya ya Chekecha Cheketua.
Shabiki wa Ali Kiba akiwa na tisheti kuonyesha kuwa yeye ni ‘Team Kiba’.
Ali Kiba akizidi kulitawala steji la kupanda na kushuka la Dar Live.
Wapiga vyombo wa Ali Kiba wakiwa kazini.
Mwanamuziki Msaga Sumu akiwarusha mashabiki wa Dar Live katika shoo ya Mwana Dar Live Sikukuu ya Pasaka.
Nyomi ikimpa shangwe Msaga Sumu.
Isha Mashauzi na kundi lake la Mashauzi Classic wakilishambulia jukwaa la Dar Live katika shoo ya Mwana Dar Live.
Isha Mashauzi akifanya yake stejini.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayefanya vizuri katika tasnia hiyo, Pamela Daffa ‘Pam D’ akiwarusha mashabiki wa Dar Live kwa songi lake kali la Nimempata.
Vijana wa Pam D wakifanya yao stejini.
Pam D akizidi kuwadatisha mashabiki.
Mshindi wa kitita cha shilingi milioni 10/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Shamila Ramadhani (kushoto) akikabidhiwa hundi yake na Balozi wa promosheni hiyo, Hillary Daud ‘JayMillions’ baada ya kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo. Katikati ni mume wa mshindi huyo Abdallah Mahoka. Makabidhiano hayo yalifanyika jana wakati wa Tamasha la Mwana Dar Live, kwenye ukumbi wa Dar Live. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Mshindi wa milioni 10 za JayMillions, Shamila Ramadhani na mumewe wakionesha mfano wa hundi ya fedha hizo.
JayMillions akipozi na baadhi ya wadau wa Dar Live sambamba na warembo alioambatana nao baada ya kutoa mahela.
MSANII wa kizazi kipya anayetamba na wimbo wa Chekecha Cheketua, Ali Saleh ‘Kiba’ amewapagawisha vilivyo mashabiki wake waliojitokeza katika shoo ya Mwana Dar Live kwenye Sikukuu ya Pasaka katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani, Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Ali Kiba akiwa sambamba na mdogo wake Abdul Kiba waliangusha bonge la burudani huku wakiimba nyimbo zao zote kwa kutumia vyombo vya jukwaani ‘live band’.
Shoo hiyo ilisindikizwa na Isha Mashauzi akiwa na Mashauzi Classic, Msaga Sumu na Pamela Daffa ‘Pam D’ ambao walitoa burudani ya nguvu na kuzikonga nyoyo za mashabiki waliofurika ndani ya ukumbi huo.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA GPL