Mwimbaji wa R&B na Pop mwenye asili ya Canada anayefanya kazi ya muziki nchini Marekani amekata ukimya wa muda mrefu kwa kuachia kibao cha “What Do You Mean”.
Justin Bieber amekuwa kimya kwa muda mrefu tangu aachie ngoma yake iliyokwenda kwa jina la Confident na sasa amerudi kuudhihirishia Ulimwengu wa muziki kuwa bado yupo vizuri.
Maneno yasiwe mengi nimeweka hapa video ya “What Do You Mean” uweze kujionea mwenyewe:
Video hii imewekwa kwenye mtandao wa You Tube siku ya tatu sasa na tayari imeshafikisha watazamaji 9,309,610.