Mtanzania Diamond Platinumz ameendelea kuchanja mbuga kunako anga ya muziki wa kimataifa baada ya kuweza kuchaguliwa kuwania tuzo za MTVEMA katika nafasi ya Mwimbaji bora wa bara la Africa.
Thanks alot @MtvEma for this, only God know how grateful and Humbled i am..🙏 @mtvbaseafrica @Mtvza pic.twitter.com/9nQxd620oF
— Diamond Platnumz (@diamondplatnumz) September 8, 2015
MTV EMA ni tuzo za muziki kwa bara la Ulaya. Katika kinyang’anyiro cha kuwania msanii bora wa Afrika Diamond anachuana na wakali wengine wa Afrika wakiwemo Wanigeria Davido na Yemi Alade na Mwafrika Kusini AKA. Hata hivyo bado una nafasi ya kumchagua msanii atakayekamilisha idadi ya wasanii kuwa watano katika kipengele hicho.Wasanii wanaochuana kumpata mmoja ni Mnigeria Wizkid, Wafrika Kusini Cassper Nyovest na KO, Mghana Stonebwoy na Mwaivory Cost DJ Arafat. Sherehe ya kutoa tuzo hizi itafanyika Octba 25 huko Milan nchini Italia.
Add your favourite musician to the Best African Act category; including #MTVEMA AND #Nominate(ArtistName) in tweets pic.twitter.com/nYOtSMCL5c
— MTV Base Africa (@MTVbaseAfrica) September 8, 2015
Muda wa kuanza kupiga kura ukifika tusisite kuileta heshima hii nyumbani Tanzania.