Mwigizaji wa Bongo movie na mkurugenzi wa kampuni ya Jerusalem Film, Jacob Stephen ‘JB’ amesema kuwa upande wake anaona sanaa inalipa kuliko siasa.
Akizungumza na Global Publishers, JB amesema kuwa kupitia sanaa ameweza kutoa ajira kwa watu wasiopungua 30 katika kila filamu anayoitoa.
“Sanaa inanilipa, sifikirii kama ubunge au siasa kwa ujumla inaweza kunilipa kama sanaa ambayo naipenda kutoka moyoni. Labda nikupe mfano, kupitia kampuni yangu, nikizalisha filamu moja inatoa ajira kwa wafanyakazi wasiopungua 30, itatoa ajira katika maduka, machinga na sehemu mbalimbali zinazouzwa filamu.”alisema JB
Aliongeza kwa kusema;
“Sanaa imetoa ajira kwa wasanii Mil 10. Unafikiri hao watu wangefanya nini kama si sanaa?,” alisema JB.
Source: GPL