Na Mwandishi Wetu.
Wazalishaji wa bidhaa zinazotozwa ushuru kwa kutumia Stempu za Kodo za Kielektroniki (Electronic Tax Stamps – ETS) wameiomba Wizara ya Fedha na Mipangopamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupunguza zaidi viwango vilivyotangazwa Jumatatu wiki hii kwa vile viwango vya sasa vya ushuru huo ni vikubwa sana.
Akizungumza na vyombo vya habari kwa niaba ya wazalishaji wanaotozwa ushuru huo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Bwana Leodegar Tenga amesema kwamba sekta binafsi inaunga mkono uanzishwaji na matumizi ya stempu za kodi za kielektroniki na kusisitiza kuwa kiwango cha gharama hizo kiwezeshe ukuaji wa viwanda nchini.
“Wenye viwanda wanaunga mkono mpango wa serikali kutekeleza matumizi ya ETS kwakuwa yanaleta usawa na ushindani sawia na kuboresha mazingira ya biashara kwa ajili yakuchochea ukuaji wa uchumi, Wanachama wa Shirikisho pia wanaunga mkono matumizi ya ETS kwa kuwa ETS inasaidia kuleta uwazi katika uendeshaji wa biashara na kupunguza undanganyifu kwenye biashara na kuondoa ongezeko la biashara haramu kwenye soko, lakini pia ushuru wa ETS unaotozwa sasa siyo tu kwamba unaongeza gharama za uzalishaji, vilevile unaathari kwenye maendeleo ya sekta ya viwanda na uchumi kwa ujumla, wenye viwanda wamewahi kuwa na majadiliano na TRA, na kuwasilisha kwa serikali mfumo mbadala kama jawabu la kupunguza kiasi kikubwa cha viwango vya gharama vinavyotozwa kwenye ETS. Hata hivyo, maombi yetu ya kuomba viwango vya gharama za ETS upunguzwe hayakuchukuliwa kabisa kufuatia kutangazwa wiki hii kwa viwango vipya vyenye mabadaliko madogo sana. ” Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa CTI
Na kuongezea kuwa CTI kwa niaba ya wenye viwanda ilishawahi kupeleka mapendekezo ya wenye viwanda serikalini ambayo yalitarajiwa yazingatiwe katika kutoa maamuzi ya kuweka viwango vipya vya gharama za ETS kutokana na Vigezo ivyo tunaomba kupitia upya na kupunguza gharama za ETS ili kupunguza athari za viwanda ambavyo vinaendelea kulipa kodi mbalimbali, wazalishaji wakiwakilishwa na shirikisho kama wadau, washirikishwe katika mchakato wa kurekebisha mfumo mzima wa ETS , Mchakato wa kutafuta mzabuni uwe wa wazi na shindani, kuwepo mpango mahususi wa kutoa huduma ya ETS kwa kutumia mfumo unaoendeshwa na sisi wenyewe, Malipo ya Stempu za ETS yafanyike kwa shilingi za Kitanzania badala ya dola za kimarekani, na mwisho Tunaomba mchakato wa kutafuta mbadala wa ETS ufanyike kukidhi vigezo vya serikali na kupunguza mzigo wa gharama za viwanda. Alimalizia Bwana Tenga.
Aidha wameipongeza Serikali kwa kuruhusu ulipaji wa gharama za ETS kwa fedha za Kitanzania na kukiri kuwa ukweli ni kwamba punguzo la gharama za ETS Haliwatii moyo wazalishaji hao wa Bidhaa za Viwandani.