Sifa ya Senegal kama ngome ya demokrasia katika eneo lisilo na utulivu iko kwenye hatari – wakati waandamanaji wakipambana na polisi nje ya Bunge la Kitaifa.
Wabunge wamepitisha mswada tata wa kuongeza muda wa rais na kuchelewesha uchaguzi kwa miezi sita baada ya Rais Macky Sall kusitisha uchaguzi uliopangwa kufanywa wiki tatu zijazo.
Khalifa Sall, mpinzani mkuu na meya wa zamani wa Dakar, alitaja kucheleweshwa huko kuwa ni “mapinduzi ya kikatiba” na kuwataka watu kuandamana. Muungano wake wa kisiasa umeapa kwenda mahakamani.
Thierno Alassane Sall, mgombea mwingine, aliita hatua hiyo kuwa ni “uhaini mkubwa” na kuwataka wafuasi wake kukusanyika mbele ya Bunge la Kitaifa kuandamana na “kuwakumbusha wabunge kusimama upande sahihi wa historia”.
Cc; BBC Swahili
#KonceptTvUpdates