Serikali imetili mkazo juu ya matumizi mazuri ya Maudhui kwa kufauata sheria ili kuepuka adha ya kuonekana Vyombo vya Habari kukosa uhuru wake maana Serikali haina mpango wa kufanya hivyo endapo utaratibu utazingatiwa.
“Nitoe wito kwa wanahabari, timizeni wajibu wenu kwa kufuata sheria, Serikali haina mpango wa kuingilia uhuru wa wanahabari kutimiza majukumu yao. Kama kuna mahali watu wanaamua kutumia content [maudhui] yoyote wafanye kwa kufuata sheria, lakini hakuna kiongozi yeyote wa serikali ambaye ana mpango wa kuingilia uhuru wa vyombo vyetu vya habari kutimiza majukumu yao.” – Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
#KonceptTvUpdates