Rais wa heshima Simba SC na Mfanyabiashara Mohammed Dewji “Mo Dewji” amefunguka kuwa amewekeza Mabilioni ya Fedha kuifanya Simba ipande viwango hadi kuwa Miongoni mwa Vilabu 10 Bora kwenye Soka Barani Afrika
“Nadhani kitu ghali zaidi nilichowahi kununua ni klabu ya mpira inaitwa Simba inamashabiki milioni 35, niliinunua hii klabu miaka mitano iliyopita, nimepoteza takribani Dola za marekani milioni 4 (Tsh bilioni 10.2) kwa mwaka mmoja na kwa miaka yote mitano nimepoteza Dola za marekani milioni 20 (Tsh bilioni 51).
“Nimeifanya Simba kuwa kwenye orodha ya vilabu 10 Bora Afrika inaleta furaha kwa watu na Afrika pia ni furaha kwangu,” Rais wa Heshima na Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji akizungumza kwenye Podcast ya Ahmed Mahmood.
#KonceptTvUpdates