Watu saba wote Wakazi wa Kijiji cha Kalambo Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa, wamehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja Jela kila mmoja na Mahakama ya mwanzo Wilaya ya Kalambo baada ya kugoma Watoto wao wenye umri kati ya miezi 9 hadi 59 wasipewe chanjo ya ugonjwa wa Surua na Rubela wakidai chanjo sio maagizo ya Mungu.
Hukumu hiyo imetolewa February 26,2024 na Mahakimu wa Mahakama hiyo Elis Mkama na Suzy Mkinga kwa Washtakiwa hao ambao ni Abiniel Isaya (27), Misheck Simon (28), Isack Simon (26), Yona Simon (30), Efeso Peter (28), Job Simon (36) na Joshua Meshack (40)
Akitoa taarifa kuhusu hukumu hiyo February 27,2024, RPC wa Rukwa, Shadrack Masija amesema chanjo hiyo ilikuwa ikitolewa na Wizara ya afya katika Kijiji hicho February 18,2024, ambapo sababu ya kugomea ni imani ya dini yao ya Kanisa la Watchtower kwamba chanjo sio maagizo ya Mungu.
RPC Masija mesema “Kugomea chanjo inayoelekezwa na Serikali ni kufifisha juhudi za Serikali za kupambana na maradhi hivyo amewahimiza Wananchi wazingatie maagizo na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Serikali na wazitii Mamlaka za Serikali kwani zimewekwa na Mungu ambaye ndiye wote tunamwabudu”
Cc; @tanpol
#KonceptTvUpdates