#MITINDO Mshiriki wa Miss World 2024 kutoka Tanzania Halima Kopwe ambaye ni Miss Tanzania 2022 amerejea nchini leo hii akitokea nchini India kushiriki mashindano ya 71 ya Miss World.
Halima alikuwa miongoni mwa washiriki 112 na alifika hadi hatua ya 40 Bora kwenye mashindano hayo yaliyofanyika Machi 9,2024, Mumbai, India.
Taji la Miss World mwaka huu 2024, limeenda kwa mlimbwende Krystyna Pyszková wa Czech Republic.