#MICHEZO; Beki mahiri wa kushoto wa Azam FC, Pascal Msindo, amejidhatiti kusalia kwenye viunga vya wana Lambalamba Azam Complex hadi mwaka 2027, baada ya kuongeza mkataba mpya wa miaka miwili.
Menejimenti ya Klabu hiyo imethibitisha kusalia kwake kupitia kurasa zake za mitandao ya Kijamii.
Msindo amekuwa na kiwango bora kwa msimu huu hadi amepata nafasi ya kuaminika, kuitwa na kucheza katika kikosi cha Timu ya Taifa “Taifa Stars”
#KonceptTvUpdates