Ikiwa
ni mda mfupi sana tangu alipoingia katika kampuni yenye wasanii kama
Dogo janja, Amazon PNC na wengineo inayojulikana kama watanashati, Suma
Mnazareti ameaschana na chama hilo linaloongozwa na ashati Ostaz Juma
Namusoma.
“Nimeamua
kujitoa mtanashati, na sababu kubwa katika zote ya kujitoa ni kwamba
nilifata kazi kwa Ostaz na sio hela zake, so nilichokuwa nadhania
ntakipata mtanashati hakipo,Boss anatafta zaidi sifa na ustaa Tanzania
na mimi mziki ni kazi yangu..anaweza akagawa mamilioni kwa watu ili
atajwe lakini anashindwa kulipa hela ya maana kwa ajili ya video,
matokeo yake anatoa shilingi laki tatu? unadhani tutaweza kushindana na
video kama za kina Ay za million 30?. nimeuza mpaka balackberry yangu
kuongeza kwenye pesa za kukamilisha video yangu, wakati hata nilivyokua
ha hustle mwenyewe sikuwahi kuuza sim yangu. so nimejiondoa maana sioni
faida yoyote, na mimi mziki kwangu ni kazi nataka nifike mbele zaidi.
aliongea Suma