Mwanadada Elizabeth Michael ama LULU leo ametembelea hospitali ya
Ocean Road Iliyopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa zawadi za
fedha kwa ajili ya wagonjwa wa cancer hospitalini hapo. kupitia ukurasa
wake wa instagram LULU ameandika
“Naamini Mimi sio mwema sana mpk Mungu akaniwezesha kuona mwezi huu
nikiwa mzima na mwenye afya…!kwa kutambua Hilo nimeanza mwezi huu kwa
kupita ktk hospital ya OCEAN ROAD na kutoa mchango ili kuwasaidia
wagonjwa wa CANCER…!Tuwe na utaratibu wa kuwakumbuka wahitaji kwa
chochote tulichonacho! Nawatakia mwezi wenye Baraka na mafanikio!…”
Hongera sana lulu kwa moyo wako huu.
CREDIT : BONGOMOVIES